Laparoscopy Semina katika Hospital ya Kairuki

Laparoscopy Semina katika Hospital ya Kairuki

Kutokana na uhaba wa huduma ya upasuaji kwa njia ya matobo nchini, madaktari wazawa takribani 200 kutoka hospitali mbalimbali nchini wameshauliwa kujifunza aina hiyo ya upasuaji itakayosaidia kupunguza gharama za wagonjwa wasiokuwa na kipato kwenda nje ya nchi kufuata huduma hiyo.

Hayo yanatokana na idadi kubwa ya wagonjwa kukimbizwa nchi za nje kufuata upasuaji wa aina hiyo, hali ya kuwa kuna baadhi ya hospitali na madaktari wenye uwezo wa kufanya huduma kama hizo, licha ya kukosekana kwa elimu ya kutosha kwa baadhi ya madaktari na wagonjwa juu ya njia hiyo ya upasuaji.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kufungua Semina ya upasuaji huo uliofanyika kwa njia ya wazi jijini Dar es Salaam jana, Kaimu Mkurugenzi wa hospitali hiyo, Dk. Muganyizi Kairuki, alisema upasuaji huo unafanyika kwenye baadhi ya hospitali na kueleza kuwa wanaamini nyingine zitakubaliana na teknologia hiyo na kuitumia.

Dk. Kairuki alitaja faida za upasuaji huo tofauti na ule wa kawaida ambao mtu hupasuliwa sehemu ya tumbo, akisema ni pamoja na mgonjwa kurudi nyumbani mara baada ya operesheni.

“Kutokana na umuhimu wa tiba hii kuhitajika nchi, tumeamua kushilikiana na baadhi ya madaktari kutoka nchi za nje kama India, China, Afrika Kusini, Namibia na Kenya ili kupeana uzoefu na mafunzo ya kufanya operesheni kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya vitundu vidogo, badala ya kuchana eneo kubwa la mwili wa mgonjwa, tumekutanisha Vidonda huwa vidogo ikilinganishwa na upasuaji wa kawaida, lakini pia mtu anafanyiwa upasuaji asubuhi jioni anarudi nyumbani,” alisema.

Ofisa Mkuu wa Tiba, kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Donan Mmbando, katika hotuba yake iliyosomwa na kaimu wake, Dk. Edwin Mng’ong’o, alisema anaamini ujenzi wa chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba cha Muhimbili utaongeza udahili kutoka wanafunzi 2,400 na kufikia 12,000 ambapo watachangia kuongeza wataalum wa upasuaji.

“Lengo la hii semina ni kuhakikisha madaktari wetu wanapata uzoefu ambao unaweza kuisaidia nchi yetu katika suala la afya, pia kuwafahamisha watanzania kwamba upasuaji huu unafanyika katika hospitali zetu na madaktari wetu wazawa. Licha ya kuwa umeanza muda mrefu lakini ulikuwa bado aujatambulishwa kama inavyotakiwa” aliongezea Mng’ong’o.

laparoscopy_training_in_kh_01_720_360_c1-1
Washiriki wakijiandikisha kabla ya kuanza kwa semina hiyo.
Daktari Bingwa wa upasuaji katika Hospitali ya Kairuki Dk. Muganyizi Kairuki akizungumza wakati wa semina hiyo.
Daktari Bingwa wa upasuaji katika Hospitali ya Kairuki Dk. Muganyizi Kairuki akizungumza wakati wa semina hiyo.
Washiriki wa semina hiyo
Washiriki wa semina hiyo
Baadhi ya washiriki wa semina hiyo.
Baadhi ya washiriki wa semina hiyo.
Mgeni rasmi akizungumza wakati wa kufungua semina ya upasuaji kwa njia ya matobo iliyowashirikisha zaidi ya madaktari 250 kutoka wazawa madaktari bingwa kutoka nje ya nchi.
Mgeni rasmi akizungumza wakati wa kufungua semina ya upasuaji kwa njia ya matobo iliyowashirikisha zaidi ya madaktari 250 kutoka wazawa madaktari bingwa kutoka nje ya nchi.
Washiriki wa semina hiyo.
Washiriki wa semina hiyo.

Chumba cha upasuaji.
Chumba cha upasuaji.
Jopo la madaktari wakimfanyia operesheni ya kuondoa mawe tumboni mmoja wa wagonjwa waliolazwa katika hospitali ya Kairuki Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Jopo la madaktari wakimfanyia operesheni ya kuondoa mawe tumboni mmoja wa wagonjwa waliolazwa katika hospitali ya Kairuki Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Madaktari wakifanya operesheni ya Laparascopic
Madaktari wakifanya operesheni ya Laparascopic
Daktari bingwa wa upasuaji kutoka Afrka Kusini, Prof. Zacharia Koto (wa tatu kulia), akisaidiana na daktari bingwa wa upasuaji kutoka Namibia Dk. S. Kaikai (wa pili kulia) wakimfanyia operesheni ya kuondoa mawe tumboni mmoja wa wagonjwa waliolazwa katika hospitali ya Kairuki, wakati wa semina ya upasuaji kwa njia ya matobo iliyofanyika katika hospitali ya Kairuki Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Mfuko wa nyongo.
Mfuko wa nyongo.
Baadhi ya washiriki wa semina ya upasuaji kwa njia ya matobo iliyofanyika katika hospitali ya Kairuki Mikocheni jijini Dar es Salaam
Baadhi ya washiriki wa semina ya upasuaji kwa njia ya matobo iliyofanyika katika hospitali ya Kairuki Mikocheni jijini Dar es Salaam

Naibu Mkurugenzi Kairuki Hospital, Clementina Kairuki (kushoto) na Dk. Najimu Mohamed wakipewa maelekezo na Daktari Bingwa wa Upasuaji, S. Kaikai kutoka Namibia (wa pili kulia) wakati wa mafunzo ya utumiaji wa vifaa vya Laparoscopic vinavyotumika kwa ajili ya kufanyia operesheni ya matobo. Mafunzo hayo yalifanyika katika Hospitali ya Kairuki jijini Dar es Salaam juzi, na kuwashirikisha madakatari kutoka ndani na nje ya nchi.

Daktari Bingwa wa Upasuaji kutoka Namibia Dk. Brown Ndofor akitoa mafunzo ya utumiaji wa vifaa vya Laparoscopic vinavyotumika kwa ajili ya kufanyia operesheni ya matobo iliyofanyika katika Hospitali ya Kairuki jijini Dar es Salaam juzi, na kuwashirikisha madakatari kutoka ndani na nje ya nchi.
Daktari Bingwa wa Upasuaji kutoka Namibia Dk. Brown Ndofor akitoa mafunzo ya utumiaji wa vifaa vya Laparoscopic vinavyotumika kwa ajili ya kufanyia operesheni ya matobo iliyofanyika katika Hospitali ya Kairuki jijini Dar es Salaam juzi, na
kuwashirikisha madakatari kutoka ndani na nje ya nchi.